MVUA ZALETA MADHARA KAHAMA
Watu 42 wamepoteza maisha na wengine 82 kujeruhiwa baada ya mvua ya upepo mkali kusababisha mafuriko katika kata ya mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi imewaacha watu 3,500
bila makazi katika kaya 350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya
mifugo ikisombwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro Rufunga amesema mvua hiyo
ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha mafuruko katika kata
ya Mwakata kuezua nyumba na nyingine kuanguka.
Amesema mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya ikiwemo mifugo kuzolewa
na maji na vyakula kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.
TUNATOA POLE KWA WANANCHI WA TANZANIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni