Jumanne, 10 Machi 2015

meter za LUKU



Natumaini ni wazima nyote, leo ningependa kuwapa faida na hasara Kuhusu hizi meter za LUKU za Tanesco, kwanza inabidi tuelewe kazi ya LUKU, Meter ya LUKU ni kifaa kinachosoma matumizi ya kiasi unachokitumia kulingana na vifaa ulivyonavyo katika nyumba, sasa kitu ambacho hutokea hapo utakuta matumizi yanaweza kuwa makubwa kuliko vifaa vyako na usiweze kujua kama ni vifaa vyako vina leakage au inawezekana luku ndo ikawa ina hitilafu,

Sasa cha kufanya hapo ni kwenda katika main switch kuizima lakini kabla ya kuizima angalia unit zako ziko ngapi ndo uzime, baada ya hapo kaa kama masaa mawili ndipo utakapoiwasha, lakini kabla ya kuiwasha cheki unit zipo ngapi, kama utaona unit zimeshuka basi cha kufanya hapo ni kumtafuta fundi umeme akufanyie checkup katika wiring yako kwani inawezekana wiring ikawa loose connection katika maungio yako, pili inawezekana kile chuma cha ethi load kikawa kimeoza ardhini nacho pia kinasababisha matumizi kuwa makubwa na vile vile tunashauriwa kuzifanyia ukaguzi nyumba zetu kila baada ya miaka miaka mitatu.

Mie ni mshauri na pia ni fundi wa umeme, 


>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

 
Kama ni fundi bado una mapungufu. 1. Ethi load ndio nini? 2. Unaposema imeoza aridhini napo pia sikuelewi maana hicho chuma ni shaba na shaba haiozi. Kitu kinachooza kinatoka wadudu je hiyo shaba inaweza kutoka wadudu. 3. Kama earth load ni haina conection umeme utaisha kwa kwenda wapi?





>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>Duuuuuuuuuuuuu>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni