ZOEZI LA KUWASAJILI WAHAMIAJI WALOWEZI
LAMALIZIKA MKOANI KIGOMA
- ZAIDI YA WAHAMIAJI WALOWEZI 20,000 WAJIANDIKISHA
- AFISA UHAMIAJI MKOA KIGOMA 'AMWAGA' SIFA KWA MAAFISA WA ZOEZI
- SHEREHE YA KUMALIZA ZOEZI YAFANYIKA HOTELINI HILLTOP KIGOMA
Akiongea na bloga wetu, Afisa kutoka shirika la Uhamaji la Kimataifa (IOM) Bi. Mia Melbeck alisema kuwa lengo lilikuwa ni kuandikisha walowzi elfu 10 lakini idadi imejitokeza maradufu. ''This was a pilot and we expected to register 10 thousands individuals but in turn a large number of people came out, we registered more than 20 thousands. I would like to thank all immigration staffs for their commitment in this exercise, they worked tirelessly in a harsh and unfriendly environment just for the benefit of their lovely country Tanzania.'' alimalizia kuongea Bi. Mia.
Naye Afisa Uhamiaji mkoa wa Kagera alisema kwamba zoezi hili ni muhimu sana kwa idara ya uhamiaji nchini kwani katika mkoa wa Kigoma walowezi waliojiandikisha kwa sasa hawatokuwa na hofu ya kufukuzwa nchini bali wataelekezwa taratibu nyingine za kufuata ili kuhalalisha ukaazi wao hapa nchini.
''Kwa kweli zoezi hili limetuwwezesha kuwafahamu nani ni nani na nani ni nani, lilikuwa ni la hiyari hivyo najua kwamba kuna wengine wengi tu ambao hawajajiandikisha. Sasa hawa wasiojiandikisha ndio watakaohusika katika oparesheni za kusaka wahamiaji haramau, hawa waliojiandikisha wao watasubiri utaratibu watakaoelekezwa badae baada ya zoezi kama hili kukamilika katika mikoa ya Geita na Kigoma.
Nao maafisa waliokuwa katika zoezi hili wamesifu namna Afisa Uhamiaji alivyoridhika na kazi walioifanya, mmoja wa maafisa hao aliyeongea na bloga wetu Bwana Orined Kaminyonge alisema ''Kwakweli tumiejisikia amani mioyoni mwetu kwa jinsi RIO (Afisa Uhamiaji Mkoa) alivyokubali kazi yetu. Na pia kuamua kutuandalia sherehe ya kutupongeza na kutuaga kwa kweli ni bonge la shukrani. Na hii inatupa morali ya kufanya kazi kwa juhudi katika mazoezi mengine yajayo.
Sherehe ya kumaliza zoezi hilo mkoani Kigoma ilifanyika katika hoteli ya Hilltop nje kidogo ya mji wa Kigoma katika ufukwe wa Ziwa Tanganyika iliwajumisha maafisa Uhamiaji na wale wa IOM ambapo Mtaalamu wa IT kutoka IOM Bwana Paata alitumia fursa hiyo kuagana na wote aliofanya nao kazi na kuwakaribisha nchini Georgia.
Katika zoezi hilo ambalo maafisa walikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo hema kung'olewa na upepo na mvua kali hali iliyosababisha Afisa Lenatus Mwambene kujeruhiwa mguuni,majanga mengine ni kupanda na kushuka milima yenye miteremko mikali, kuvuka mito kwa mitumbwi na kula au kulala katika mazingira magumu.
TUWAPONGEZE MAKAMANDA WETU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni