Mchinjaji wa IS..... 'Jihadi John' atambuliwa
Mwanaume ambaye
amekuwa akitekeleza mauaji ya mateka wa kundi la wapiganaji wa Islamic
State ajulikanaye kwa jina la utani "Jihadi John",ametambuliwa.
Bwana huyo ambaye taswira yake akiwachinja mateka kwa kisu bila huruma
ndiyo nembo ya wapiganaji hao sasa ametambuliwa kuwa anatokea Uingereza.
Shirika la Habari la BBC limetambua kuwa jina lake kamili ni Mohammed Emwazi.
Emnuazi ameonekana kwenye video kadhaa ya mauwaji ya mateka wa mataifa
wa magharibi, akiwemo Mmarekani James Foley, Raia wa Uingereza, Alan
Henning na mwaandishi habari wa Japan, Kenji Goto.
Inaaminika kuwa Emwazi ni raia wa Uingereza na hasa anatokea magharibi mwa London.
Yamkini Emnuazi aliyezaliwa Kuwaiti na mwenye umri wa kati ya miaka 20
-29 alikuwa amefahamika sana na vyombo vya usalama lakini kwa sababu za
kiusalama haikuwezekana kumtambua.
Anaaminika amewahi kuishi Somalia mnamo mwaka 2006 na anauhusiano mkubwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabab nchini humo.
Polisi nchini Uingereza imeziomba vyombo vya habari kutosambaza habari
ambazo hawajazithibitisha kumhusu jamaa huyo kwani uchunguzi unaendelea.
Hata hivyo bado habari za kina kumhusu Jihadi John hazijatolewa.
Mwandishi wa maswala ya Usalama wa BBC Tomi Oladipo anasema kuwa vyombo
vya usalama vya serikali za mataifa yanayokaribia Somalia sasa yana
kila sababu ya kutahamaki.
Bwana huyo aliwahi kushirikiana na kundi la Al Shaabab
Kwa sababu Kuhusika kwake na kundi la Al Shaabab kisha akajiunga na
kundi la Islamic State ambalo kwa wakati mmoja lilikuwa linashindana na
wanamgambo wa Al Qaeda kuhusu yupi kati yao anayeushawishi
mkubwa
Ishara kuwa Al Shabab inazingatia msimamo mkali wa kidni hata zaidi ya Al Qaeda.
Kwa sababu itakumbukwa kuwa Al Qaeda ilipinga hatua kali ya kuwachinja mateka nchini Iraq na Syria.
Emnuazi ambaye amekuwa akiwabeza mataifa ya Magharibi kabla ya kuwakata
shingo naaminika kuwa mtaalamu wa maswala ya kompyuta alisomea chuo
kikuu cha Westminster.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC bwana huyo
anaaminika kuwa alikwenda Syria mwaka wa 2012, lakini kabla ya wakati
huo majasusi wa Uingereza na Marekani walikuwa hawajajua tishio lake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni