Wakaazi wa wa Endarasha, kaunti ya
Nyeri, wanaishi kwa mashaka makubwa kutokana na Nyani na tumbili
wanaofugwa katika hifadhi ya taifa la Kenya ambayo iko jirani na makaazi
yao,ambao huwashambulia na kuwanyanyasa wanawake tu.Katika tukio la hivi karibuni mwanamke mmoja alishambuliwa na nyani wa kiume wapatao kumi .walikuwa na kitisho kikuu,hufungua midomo yao na kuunguruma huku wameshikilia tupu zao huku wakimtishia anaeleza mwanamke aitwaye Wangui.
Mwanamke mwingine alishambuliwa na kuvuliwa nguo zake wakati alipokuwa akijaribu kuwazuia nyani hao wasivamie shamba lake .
Na
wanaume upande wao wanalielezeaje tukio hili? John Kariuki anasema
kwamba jamii hiyo ya wanyama inazidi kuongezeka kwakuwa wanapata chakula
cha bure kutoka mashambani na huko kwenye hifadhi hawapati chakula cha
kutosha.Jambo kubwa zaidi linalofanya wanyama hao waongezeke kwa kasi ni kwamba, mmoja wao akizaa huzaa pacha.na wanadamu si wengi kiasi hicho kijijini hapo,na wanajibidiisha zaidi katika kilimo lakini hawapati mazao ya kutosha,anaeleza Kariuki.
Endarasha Peter Kamau ametoa wito wa kutafutwa kwa suluhisho la haraka kabla wakaazi hao hawajachukua sheria mikononi mwao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni