Jumanne, 10 Machi 2015

ULIZA UJIBIWE............

 

Kwanini Ndege (Roketi) huacha mstari wa Moshi?

Inavyoeleweka huku angani kuna upepo wenye kasi kubwa (marekebisho kama siko sahihi).

Mara nyingi nimeona zile ndege zinazopita juu sana zamani tukiziita 'roketi' zinaacha mstari mweupe wa moshi na mstari huu unachukua muda kupotea/kutawanyika unaweza kuchukua hata dakika 10 au zaidi.

Je, kwa nini hali hiyo inatokea au inawezekana kuwa si kweli kuna upepo mkali huko angani?????
 
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
 

Kwa Nini Ndege (Roketi) Huacha Mstari Wa Moshi?

>>>>> Kwanza umeshawahi kupanda ndege? Ndege zinaporuka anga za mbali, e.g. KLM inapofika anga za juu, kule kuna baridi sana kiasi cha kufikia -50 Centigrade au zaidi. Kinachotokea ndege inapotoa moshi ule unakutana na mgandamizo mkubwa sana na baridi sana kiasi kuwa ule moshi unagandishwa ghafla.

Umeshawahi kujiuliza unapoamka asubuhi sana sehemu za baridi sana,. hewa unayotoa wakati unapumua kwa nini inakuwa kama moshi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni