Wanasayansi
wamegundua taya wanaodai ni ile ya mtu wa kwanza duniani.
Kiolezo
hicho chenye miaka millioni 2.8 kina miaka 400,000 zaidi ya ugunduzi wa utafiti
unaosema kuwa mtu wa kwanza alitokeza.
Ugunduzi
huo uliofanyika nchini Ethiopia unasema kwamba mabadiliko ya hali ya hewa
yaliathiri maumbile ya binaadamu aliyetegemea miti hadi akaanza kutembea wima.
Mkuu
wa kundi la utafiti ameiambia BBC kwamba ugunduzi huo unatoa ufahamu wa kwanza
kuhusu mabadilio muhimu ya binaadamu.
Proffessa
Brian Villmoare kutoka chuo cha Nevada mjini Las Vegas amesema kuwa ugunduzi
huo unatoa uhusiano kati ya binadaamu anayefanana na nyani kwa jina Lucy
aliyeishi miaka millioni 3.2 ilioipita na ambaye aligunduliwa mwaka 1974 katika
eneo hilo.
Ehtiopia
Je,
Lucy aliyefanana na maumbile ya binaadamu ana uwezo kuwa alibadilika na kuwa
binaadamu wa kawaida?
Lakini
rekodi ya taya hiyo kati ya mda ambapo Lucy na nduguze waliishi na kutokea kwa
mtu aliyekuwa na maumbile ya nyani aliyekuwa na ubongo mkubwa miaka millioni 2
iliopita imepishana kwa miaka mingi.
Taya
hiyo ya chini ya mdomo ilio na miaka millioni 2.8 ilipatikana na mwanafunzi
raia wa Ethiopia Chelachew Seyoun katika eneo la utafiti la Ledi-Geraru,katika
jimbo la Afar.
Ameaimbia
BBC kwamba alishangazwa alipokiona kifusi hicho.
''wakati
nilipokipata kifusi hicho ,nilijua kwamba kina umuhimu mkubwa kwa kuwa huu ndio
wakati unaowakilishwa na mabaki ya watu wa zamani mashariki mwa Afrika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni