
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete
ameamrisha kuundwa kwa kamati maalum kutoka katika upande wa serikali,
watu wenye ualbino pamoja na jukwaa la tiba asilia haraka iwezekanavyo
ili kuhakikisha kamati hiyo itashughulikia ipasavyo matukio ya utekaji
nyara na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayoendelea nchini
Tanzania. Hapo jana rais kikwete alishindwa kuonana na ujumbe wa watu
kumi na nane kwa wakati maalum uliopangwa kutokana na baadhi ya watu
wenye ualbino kuanzisha vurugu ukikataa ujumbe huo kwa madai kuwa muda
wa kukaa madarakani kwa viongozi wa chama cha watu wenye ualbino TAS
umekwisha muda wake. Kwa taarifa zaidi sikiliza matangazo yetu ya leo
mchana.
EEEEMUNGU WANUSURU NDUGU ZETU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni