Jumatatu, 9 Machi 2015

nakosa uhuru katika nchi yangu


 
 

nakosa uhuru katika nchi yangu, wananiwinda waniue, nimekua sina amani ktk moyo wangu, giza linapoingia nakua na mashaka na maisha yangu .nafungiwa kama mfungwa eti kulinda usalama wangu, nakosa uhuru wa kujumuika na wanajamii wenzangu, nashindwa kutimiza ndoto zangu kwa kuhofia maisha yangu, namhofia hata baba yangu anaweza kuniua na kuchukua viungo vyangu mama yangu ndio tumaini langu , serikali haini jali, jamiii nayo imenitenga yena inataka kuniua,

mimi albino nikimbilie wapi ili niishi kwa amani na upendo?
mim albino naitaji kuishi kama wewe
mimi albino naitaji kutimiza ndoto zangu kama wewe
mimi albino naitaji kuwa huru kama wewe
mim albino naitaji kupata elimu bora kama wewe .

Naitaji kua na furaha kama wewe
Naitaji nifurahie uumbaji wa Mungu wangu

Eeeh Mwenyezi Mungu nisikie kilio changu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni